Wednesday, February 20, 2013

STREET SCIENCE OF TANZANIA

KARIBU STREET SCIENCE OF TANZANIA 
Streat science of Tanzania ni kampuni iliyoanzishwa kwa ajili ya kutoa huduma kama vilekuunda inveter , incubator , charge, welding Biogas , Biomass n.k streat inatoa ushauri wa kiufundi pamoja na kufundisha teknolojia zana mbali mbali na kwa njia ya mtandao .Hata hivyo streat science itakuonyesha teknolojia za zamani na soda namna ya kutengeneza / kuunda . Wajiifunza kutengeneza vitu kama friji lisilotumia umeme , namna ya kutengeneza majiko yasiyotumia mkaa mwingi / kuni majiko yanayotumia oil chafu , namna ya kulihifadhi nataka kwa njia ya asili . utajifunza namna y a kutengeneza sabuni . Streat science of Tanzania itaendelea kukuletea teknolojia itakuja kwa wakati na ukihitaji iliyoundwa basi utaipata .Kila swali utakalouliza ni lazima utajibiwa na hasa linalohusiana na ufundi.


JIFUNZE KUTENGENEZA FRIJI LA ASILI LA KUPOOZESHA MAJI NA HASA SEHEMU ZENYE JOTO
Friji hili huweza kupoozesha maji kwa kiwango cha kawaida . Maji hata kama yana joto kiasi gani utaweza ukafanya yakawa na ubalidi . Hali tumii umeme na ni teknolojia ya miaka mingi . Streat Science of Tanzania inakuletea jinsi ya kulitengeneza .
VIFAA.
  1. Tafuta dumu / guduria la lita tano
  2. Tafuta magunia matatu / yaani gunia za kuhifadhia mahindi na si mifuko ya safleti
  3. Tafuta kamba ya katani / yaani zinazotumika kushonea magunia.
  4. Sindano ya kushonea magunia
JINSI YA KUTENGENEZA
  1. Valisha guduria /magunia /valisha mara ya kwanza na uashone . fanya hivyo mara tano . Kila unapovalisha hakikisha unashona vizuri yaani utashona mara tano mpaka utahakikisha dumu halionekani kabisa ila utaacha sehemu ya mdomo wa dumu kwaajili ya kuingiza maji na kufungua kifuniko cha dumu.
JINSI YA KUTUMIA
  1. Jaza maji yako ya kunywa ndani ya hilo dumu uliloshonea magunia . Hakikisha umelisafisha vizuri .
  2. Funga mfuniko wa dumu na chukua maji lowanisha dumu lote na hakikisha magunia ulioshonea yamelowa .
  3. Weka dumu sehemu yenye hewa kama ni ndani karibu na dirisha au mlango.
  4. Weka maji yako kila jioni na asubuhi au huo usiku baada ya masaa manne maji yako tayari kunywa na kama familia ni kubwa basi tengeneza dumu la lita ishirini ila gunia utashonea mara kumi.
  5. Ifikapo asubuhi mwagia tena maji yaani hakikisha gunia lako ni bichi mda wote .
NB. Maji haya si ya baridi kama friji la kawaida au mafriji ya umeme bali maji yanakuwa na baridi ya kutosha kukata kiu na ni bora kwa afya kwani yanaendana na hali ya hewa . Ukiwa na swali au maoni au kama mahali hujaelewa basi Street Science Tanzania iko tayari kukuelezea . Endelea kusoma kwani sayansi zote za asili zisizo na gharama nitaendelea kukuletea.
Kwa wale wenye mitungi iliyofinyangwa kwa udongo wakifanya hivyo basi itakuwa ni bora zaidi.

KAZI NYINGINE TUZIFANYAZO

1. kutengeneza/kuunda mashine za inverter:

mtaalam wa uundaji mashine tofauti akiwa anaunda mashine ya inverter

hizi hazili betri au zinakaa na betri muda mrefu kwa wale wenye inverter zinazokaa na betri kwa muda wa masaa 4 basi za kwetu ni imara mara tatu 
yake


2. tunaunda betri charge za kuchaji betri


3. tunaunda welding mashine



4. tunaunda incubator mashine: ni mashine za kutotolesha vifaranga zinaanzia vifaranga 100 hadi 10000



5.  tunaunda umeme kutokana na kinyesi cha ng'ombe yaani BIOGAS


6. Tunaunda umeme wa mvuke yaani steam engine

mtaalam wa uundaji wa mashine kama anavyoonekana katika uundaji wa mashine, hii ni moja ya kazi zinazofanywa na streetscience of tanzania


LEO FOCUS LEO
P.O.BOX 55909
email:streetsciencetz@gmail.com
visit:streetsciencetz.blogspot.com
www.facebook.com/pages/Street-Science-of-Tanzania
location: dar es salaam


(c)2013 all rights reserved

 

1 comment:

  1. nashukuru kwa huduma zenu nzuri,mimi niko hapa dar nataka kujifunza namna ya kutengeneza incubator na friji ,hivyo nataka kujua utaratibu wenu ukoje,mob.0763836397 na email chescoashery3@gmail.com

    ReplyDelete